Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Gérard Araud, aliyewahi kuwa balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, Marekani na Israel, akizungumzia uwezo wa kidiplomasia na kijeshi wa Iran amesema:
“Wairani ni miongoni mwa wapatanishi wa kutisha zaidi niliowahi kuwaona. Wanaweza kuendelea na mazungumzo kwa saa nyingi na ni werevu sana.”
Ameongeza kuwa Iran ni taifa lenye historia ndefu na diplomasia ya kina, na haiwezekani kulilazimisha kujisalimisha kwa mashambulizi ya anga. Araud pia ameonya kwamba Iran ina uwezo wa kulenga kambi za Marekani na hata Tel Aviv, na kinachoendelea sasa ni mchezo wa pande mbili wa kuzuia na vitisho (deterrence and threat) ndani ya muktadha wa mazungumzo.
Kwa mujibu wa mwanadiplomasia huyo wa Kifaransa, katika hali bora zaidi, Marekani haitafanya zaidi ya kurejea kwenye makubaliano yale yale ambayo yenyewe ilijiondoa mwaka 2018.
Your Comment